Connect with us

Makala

Azam Fc Yarudi Kileleni

Klabu ya Azam fc imerudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya jana kuifunga klabu ya Dodoma jiji Fc kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Mabao ya Azam Fc yaliwekwa kambani na Mkongwe Agrrey Morris dakika ya 47 huku Ayoub Lyanga akifunga kwa shuti kali dakika ya 58 na dakika ya 62 mchezaji wa Dodoma jiji Fc alijifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira.

Azam fc imerudi kileleni mwa ligi ikiwa na alama 25 baada ya kucheza michezo 10 huku Yanga sc ikiwa katika nafasi ya pili na alama 23 na Simba sc wakishika nafasi ya tatu kwa alama 19 huku mchezo baina ya watani wa jadi utaamua endapo Yanga atarudi kileleni ama la.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala