Connect with us

Makala

Azam Fc Ugonjwa Ule Ule

Licha ya kufanya mabadiliko kadhaa katika benchi la ufundi la klabu ya Azam Fc bado timu hiyo imeshindwa kupata matokeo stahiki baada ya jana kulazimishwa sare a mabao 2-2 na Ruvu Shooting katika uwanja wa Chamazi.

Danny Lyanga alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 34, bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kuwafanya vijana wa Charles Mkwasa kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao moja lakini dakika ya 53 kipindi cha pili Ruvu Walisawazisha kupitia kwa Emmanuel Martin.

Mudathir Yahaya alijibu mapigo baada ya kufunga bao la pili dakika ya 60 lakini dakika 10 baadae Fully Maganga alisawazisha na kuleta simanzi kwa timu nzima ya Azam Fc ambao wamefikisha alama 29 katika michezo 16 waliyocheza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala