Connect with us

Makala

Arteta Anaamini Kubaki Kwa Auba Emirates

Kocha mkuu wa Arsenal,Mikel Arteta anaamini kuwa mshambuliaji wake namba moja Pierre Emerick Aubameyang atasaini dili jipya Emirates kwani hii ni timu yake bora na wakiwa pamoja watafanya mambo makubwa.

Arteta ameongoza kikosi chake kutwaa mataji mawili mfululizo ikiwa ni pamoja na ule wa Kombe la FA ambapo aliichapa Chelsea mabao 2-1 na taji la ngao ya jamii kwa ushindi wa penalti 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1.

Aubameyang ndiye aliyefanikisha kutwaliwa kwa mataji hayo baada ya kufunga mabao 3 pekee kwenye michezo yote miwili,moja ikiwa ni lile la sare na Liverpool na mawili aliyowapa kichapo Chelsea kwenye kombe la FA.

Msimu mpya wa ligi kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12 na mabingwa watetezi wakiwa ni Liverpool wenye uwanja wao maarufu kama Anfield.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala