Connect with us

Makala

Aguero Kusepa Man City

Mshambuliaji  wa Manchester City, Sergio Aguero anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho pale mkataba wake utakapofika tamati mwaka 2021 na inaelezwa kuwa ana mpango wa kurejea kwenye klabu yake iliyomkuza ya Independiente ya Argentina.

Nyota huyo raia wa Argentina mwenye miaka 31 alijiunga na Manchester City akitokea klabu ya Atletico Madrid alikodumu kuanzia msimu wa 2006-2011.

Aguero ametupia jumla ya mabao 254 na ndiye namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi Kuu England.

Manchester City inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu England ikiwa na pointi 57 katika michezo 28,imeshinda mechi 18 na kutoa sare 3 .

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala