Timu ya Real Madrid walikuwa tayari kumlipa Jose Mourinho £12m ili asikubali kurudi kuifundisha timu hiyo wakati akisubiri kuondolewa kwa Zinedine Zidane, lakini mreno huyo alipenda kujiunga Tottenham . (Sun)
Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 30 , anawaniwa na Inter Milan na huenda akasajiliwa na timu hiyo katika dirisha dogo la mwezi januari. (Star)
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 27, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Brazil anayechezea kwa mkopo Bayern Munich akiwa ametokea Barcelona ana matumaini ya kusalia katika klabu ya BayernMunich ,Ujerumani . (Marca)
Ndoto za kiungo wa QPR ya England, Eberechi Eze mwenye miaka 21 kuhamia Tottenham zimefutika baada ya kocha Mauricio Pochettino kutimuliwa . Chelsea, Leicester na West Ham pia wanamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo.
Kiungo wa kati wa kimataifa wa Tottenham na Argentina Giovani lo Celso, mwenye miaka 23 anayecheza kwa mkopo Spurs kutoka Real Betis, anataka kuhamia timu nyingine (Marca)
Liverpool na Manchester United pamoja Manchester City wanamuwinda mchezaji wa Ufaransa anayechezea Lyon, Mathis Rayan Cherki, mwenye miaka 16, ambaye tayari amecheza ligi ya mabingwa ulaya na ligi ya Ufaransa. (90 Min
Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amemsifia mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish kwa ubora aliouonyesha walipocheza dhidi ya timu yake na anataka kumuwania kumsajili kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 24. (Metro)
Mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici amebainisha kuwa vibibi vizee vya Turin havina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, 31. (Mail)
Wakati huohuo Juventus bado haijaamua kuwauuza wachezaji wake mturuki Merih Demiral, 21 pamoja na Daniele Rugani, 25 ambao wamehusishwa kuwaniwa na vilabu kadhaa vikiwemo Manchester United, Manchester City na Arsenal . (Calciomercato)
Wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Uturuki anayeichezea Leicester Caglar Soyuncu, 23, amehusishwa kujiunga na Manchester City, amesema mchezaji huyo hana nia ya kuondoka King Power hivi karibuni (Leicester Mercury)
Barcelona ingeweza kumnasa kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Weigl ili kuongeza nguvu katika eneo lao la kiungo, Barcelona wako tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 21 kumnasa kingo huyo anayekipiga Borussia Dortmund (Mail)
Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 27 anataka kumaliza soka lake akiwatumikia Magpies na ameeleza matamanio yake ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo . (Newcastle Chronicle)
Klabu ya Aston Villa inahusishwa na kutaka kumsajiri winga wa kifaransa Romain Alessandrini, 30. (Birmingham Mail)
Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino ametembelea klabu ya Newell’s Old Boys ya nchini kwao Argentina – klabu yake ya kwanza kuichezea kati ya mwaka 1989 na 1994 – wakati akifikiria muelekeo wake mpya. (Mail)
Kiungo wa Atalanta Dejan Kulusevski, ambaye yuko kwa mkopo kwenye klabu ya Parma msimu huu lakini anahusishwa na vilabu vya Arsenal, Manchester United na Tottenham, ameelezea kuwa yeye ni mshabiki mkubwa wa klabu ya Chelsea. (Talksport)
Chanzo;BBc,Mitandao ya kijamii