Connect with us

Soka

Algeria wabanwa,Nigeria yaichapa AFCON 2021

Michuano ya kombe la Mataifa Afrika(AFCON) imeendelea jana nchini Cameroon kwa michezo kadhaa kupigwa siku ya jana huku miamba mikubwa ikishuka dimbani.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Algeria walishuka dimbani mapema kucheza dhidi ya Sierra Leone huku wakipata matokeo ambayo hawayakutarahia baada ya kwenda sare ya bila kufungana.

Licha ya kuwa na mkusanyiko wa vipaji vya kutosha wanaocheza ligi kubwa barani Ulaya wakiongozwa na nahodha wao Riyadh Mahrez wa Man city lakini bado hawakufua dafu,mlinda mlango wa Sierre Leone Mohammed Nbalie Kamara aliibuka shujaa wa mchezo huo kwa kuokoa mipira ya hatari iliyopigwa langoni mwake na hatimaye kuibuka mchezaji bora wa mchezo huo.

Mafarao Misri wakiongozwa na mchezaji anayewania tuzo ya dunia ya FIFA Mohamed Salah baada ya kuiona cha moto kutoka kwa Super Eagles walioibuka na ushindi wa 1-0.Mshambuliaji wa Leicester city Kelechi Iheanacho alilipatia Taifa lake Nigeria pointi tatu muhimu kwa bao safi dakika ya 40.

Michuano hiyo itaendelea tena hii leo kwa michezo mingine ambapo Tunisa watakutana na Mali,Mauritania dhidi ya Gambia na Guinea ya Ikweta dhidi ya Ivory Coast.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka