Connect with us

Soka

Nkane atua Jangwani

Winga hatari kutoka Biashara United Denis Nkane amejiunga rasmi na mabingwa wa kihistoria nchini Yanga baada ya kukamilisha usajili wake katika klabu hiyo na kutangazwa rasmi.

Nkane anasifika zaidi na uwezo wake wa kucheza winga zote mbili kutokana na kasi yake pamoja na ufundi wa kuuchezea mpira kwa kuwatoka mabeki ni kitu kinachomfanya akizi vigezo vya aina ya mawinga ambayo klabu hiyo imekuwa nao huku akifananishwa zaidi na Mrisho Ngasa.

Huu ni usajili rasmi wa tatu ndani ya kikosi hicho baada ya ule wa SalumAbubakar ‘sure boy’ na golikipa kutoka Mtibwa sugar Aboutwalib Mshery,huku pia wakihusishwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa winga kutoka TP Mazemba Chiko Ushindi.

Baada ya kusajiliwa Yanga mchezaji wa zamani wa timu hiyo Mrisho Ngasa alitumia ukurasa wake wa Instagram kummpongeza kinda huyo wa miaka 18 na kumtakia kila la kheri katika safari yake hiyo huku akimsisitiza kuzidisha nidhamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka