Connect with us

Soka

Man Utd yavuna pointi 3 kwa Burnley

Mashetani wekundu Manchester United United imepata pointi tatu muhimu kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza na kumaliza mwaka vizuri baada ya kupata ushindi mzuri wa 3-1 dhidi ya Burnley.

Katika mchezo huo uliofanyika katika dimba la Old Trafford Man Utd ilipata magoli yote matatu kipindi cha kwanza,huku pia lile la kufuatia machozi likipatikana pia kipindi cha kwanza.

Goli la kwanza liliwekwa kimiani na kiungo Scott McTominay wa shuti kali dakika ya 8 tu ya mchezo,Jadon Sancho aliiandikia timu hiyo goli la pili dakika ya 27 baada kuwachambua vizuri mabeki kabla ya Cristiano Ronaldo kuwanyanyua tena mashabiki dakika ya 35 akimalizia vizuri uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.

Burnley walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa winga wao hatari Aaron Lenon dakika ya 38 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa kati wa Man Utd.

Man Utd wamepanda hadi nafasi ya sita wakiwa na pointi 31,pointi 4 nyuma ya Arsenal walio katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo pendwa zaidi ulimwenguni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka