Connect with us

Soka

Sure Boy ni rasmi ya Wananchi

Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga sc wamemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa zamani wa Azam fc Salum Abubakar ‘sure boy’ ikiwa ni kama zawadi kwa mashabiki,wanachama na wapenzi wa klabu hiyo katika kuelekea sikukuu ya Christmas.

Usajili huo unakuwa ni wa kwanza kwa klabu hiyo katika dirisha hili dogo la usajili huku wakihusishwa kukaribia pia kumtangaza winga machachari wa Baishara Denis Nkane ndani ya timu hiyo wikiendi hii.

Salum Abubakar amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa rasmi barua ya kuvunjwa mkataba na waajiri wake wa Azam fc siku ya Jumatano,na kusajiliwa kwake Yanga ni kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kuichezea timu hiyo ambayo iliwahi kutumikiwa na baba yake mzazi mzee Abubakar Salum miaka ya nyuma.

Sure Boy anaenda kuongeza ubora na ushindani wa namba katika eneo la kiungo la Yanga lililojaa utajiri mkubwa msimu huu,na changamoto kubwa kwake ni kuhakikisha anamshawishi kumweka benchi Fei Toto au Khalid Aucho walio kwenye ubora mkubwa tangu kuanza kwa ligi.

Yanga inatajwa kuwa itafanya sajili tatu mpaka nne katika dirisha hili huku usajili wa golikipa ukiwa ni jambo muhimu kutokana na kuondoka kwa mlinda mlango namba moja Djigui Diarra kwenda AFCON akiwa na timu ya taifa lake Mali.

 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka