Connect with us

Soka

Simba kutema watano dirisha dogo

Uongozi wa klabu ya Simba unatajwa kuachana na nyota wake watano katika dirisha hili dogo l a usajili ili kupisha kuingia kwa majembe mengine mapya ndani ya kikosi hiko.

Wachezaji hao ni golikipa Jeremia Kisubi,beki mzoefu wa kati Serge Wawa,kiungo mkabaji Abdul Swamadu na mawinga Pape Ousmane Sakho  na Jimmyson Mwinuke ambao wamekosa nafasi za kucheza kikosi cha kwanza.

Simba wanataka kupunguza mchezaji mmoja wa kimataifa ili kujaribu kumrudisha kiiungo fundi Clatous Chota Chama anayetajwa kutaka kuondoka katika klabu yake ya sasa ya RS Berkane ya Morocco kutokana kukosa furaha na kutoridhishwa na mazingira ya nchi hiyo.

Hata hivyo mabingwa hao watatetzi wa ligi kuu watakutana na upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Yanga ambao nao wapo mbele katika kuitaka saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Zambia.

Simba inasemekana wameshamalizana na kiungo wa Azam Fc Mudathir Yahya kwenda kukipiga Msimbazi akienda kuchukua nafasi ya kiungo wa zamani wa Kagera sugar Abdul Swamadi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka