Connect with us

Soka

Chelsea Yaipiga Juventus 4-0

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuifunga Juventus Fc mabao 4-0 katika mchezo wa michuano ya klabu bingwa barani ulaya(Uefa) uliofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge huku timu hiyo ikfanikiwa kuonyesha kiwango kizuri katika dakika zote za mchezo huo.

Trevo Chalobah aliifanya Chelsea kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1 baada ya kufunga bao hilo dakika ya 25 huku Reece James akiongea wenyeji bao la pili dakika kumi baada ya kipindi cha pili kuanza na Callum Hudson-Odoi aliongeza bao la tatu dakika tatu baadae huku dakika za mwishoni za nyongeza Timo Warner aliongeza bao la 4 na kuifanya timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano ikiwa na alama 12.

Ushindi huo wa Chelsea umehitimisha safari ya Zenit na Malmo katika kundi H ndani ya michuano hiyo baada ya kuwa na alama ndogo huku Juventus wakiungana na Chelsea hatua ya Mtoano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka