Soka
NDUGU YAKE NA MEDDIE KAGERE AMWAGA WINO YANGA
Imefahamika kuwa winga hatari wa kulia na kushoto anayekipiga Klabu ya Mukura Victory Sports ya Rwanda, Patrick Sibomana, usiku wa kuamkia juzi alipanda ndege ya Rwand Air na kutua nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera aliwahi kuliambia Gazeti la Championi kuwa yupo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji sita wa kimataifa watakaokuja kuichezea timu hiyo kutoka Rwanda, Nigeria, Ivory Coast na Guinea.
Hiyo yote ni katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga imepania kuuchukua ubingwa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti la Championi limezipata zinasema kuwa winga huyo amekuja kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo.
“Muda mrefu Yanga walikuwa wanamuwania winga huyo tangu msimu uliopita, baada ya kushindikana kukamilisha usajili wake.
“Lakini msimu huu wamepanga kumsajili katika kukamilisha ripoti ya kocha aliyoitoa ya kukamilisha usajili wa kila mchezaji ana..