Connect with us

Soka

Miquissone kutua Al Ahly

Mshambuliaji wa Simba na timu ya Taifa ya Msumbiji Luis Miquissone huenda akajiunga na mabingwa wa klabu bingwa Afrika Al Ahly ya Misri.

Al Ahly wameonesha nia ya dhati kumnunua mchezaji huyo ambaye anahitajika sana na rais wa klabu hiyo Mahmoud El Khatib na wako tayari kupeleka ofa inayokadiriwa kuanzia bilioni mbili za Kitanzania ambayo wanaamini itatosha kumnasa Mmakonde huyo.

Mchezaji huyo pia alikuwa anahitajika na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,lakini wamejitoa baada ya kusikia ofa ya Al Ahly kwani wao hawako tayari kulipa kiasi wanachotaka kutoa Wamisri hao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka