Connect with us

Soka

Yanga sc Yakomaa na Asukile

Klabu ya Yanga imesema itachukua hatua kali kwa mchezaji Benjamin Asukile, endapo akishindwa kuthibitisha madai yake kuwa kuna baadhi ya viongozi waliowapigia simu baadhi ya wachezaji wa Tanzania Prisons kwa madai ya kutaka kutoa pesa kiasi cha Sh. milioni 40 ili wacheze chini ya kiwango.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema kuanzia jana walikuwa kwenye harakati za kuziandikia mamlaka husika kutaka mchezaji huyo ahojiwe na apeleke ushahidi ili hatua zichukuliwe kama kuna baadhi ya watu walihusika na hilo na kama alikuwa anaongea kwa kuichafua klabu ya Yanga, basi watachukua hatua za kisheria dhidi yake.

“Sisi tumemsikia, ni kauli inayoelekea kuichafua klabu yetu ya Yanga, anataka kuonyesha kuwa sisi tusingeweza kuishinda timu yao bila kuwatafuta. Yaani timu yao ni bora sana kuliko Yanga? Wao walifungwa na Ihefu hivi karibuni kwani walihongwa? Yanga ina unyonge gani wa kushindwa kuifunga Prisons?” Alihoji Bumbuli.

Alisema hawatokubali kulinyamazia jambo hili kwa sababu maana ya mchezaji huyo ni kutaka kuiharibu nembo ya klabu na kuonekana kuwa timu yao haiwezi kuwafunga mpaka watoe kitu fulani.

Cc:Yangaapps

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka