Connect with us

Soka

Nyoni,Kennedy Mambo Safi Simba sc

Baada ya kumalizana na mabeki wa pembeni kwa kuwaongezea mikataba sasa klabu ya Simba sc imemalizana na mabeki wa kati Erasto Nyoni na Kennedy Juma ambao mikataba yao iko mwishino kumalizika.

Inadaiwa tayari makubaliano ya kuongeza mikataba mipya ya mabeki hao imeshafikiwa na kilichobaki ni kukamilisha baadhi ya taratibu ili wasaini mikataba hiyo ili kuendelea kukipiga katika klabu hiyo inayoelekea kutwaa taji la ligi kuu nchini kwa mara ya nne.

Awali zaidi ya mastaa sita walikua mbioni kumaliza mikataba klabuni hapo na hivyo kufanya kuwepo na minong’ono mingi juu ya uzembe wa uongozi kutowapa mikataba wachezaji hao hivyo kufikia makubaliano hayo ni habari njema kwa mashabiki waklabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka