Connect with us

Soka

Khama Biliat Kuikosa Simba sc

Nyota wa Kaizer Chief Khama Billiat atakosa mechi zote za ligi zilizosalia pamoja na mechi za klabu bingwa kutoka na majeraha aliyoyapata jumapili iliyopita katika mechi dhidi ya timu yake ya zamani ya mamelod sundown katika mchezo ambao Kaizer chief iliibuka na ushindi wa goli 2-1.
Billiat amepata majeraha ikiwa ni wiki chache toka atoke kupona majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu toka mwezi January.
Billiat hakucheza michezo 5 ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi, akiwa ametoka kwenye majeraha alicheza mechi ya klabu bingwa dhidi ya Horoya ya Guinea ambapo Katika mchezo huo Kaizer Chief walikuwa wametanguliwa kufungwa goli 2-1 lakini nyota huyo alifunga goli la jioni kabisa la kusawazisha na kufanikiwa kuinusuru Kaizer Chief na kipigo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Akiongea kwa masikitiko kocha wa Kaizer Chief alisema “Inasikitisha kuona mchezaji mwenye ubora kama Khama Billiat anatoka kwenye majeraha halafu anapata tena majeraha “

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka