Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 24, 2021 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kufanya maamuzi yafuatao
Mechi Namba 47A
Majimaji FC 2-2 African Sports FC Timu ya Majimaji FC imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la mashabiki wake kuruka uzio wa uwanja na kumzonga mwamuzi katika mchezo uliochezwa Februari 20, 2021 kwenye uwanja wa Amani Mkoani
Njombe.
Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 45(1) ya Ligi Daraja la
Kwanza kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Shutuma za Makamu Mwenyekiti wa Young Africans SC kwa TFF, Bodi
ya Ligi, Kamati ya Waamuzi na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa
Ligi.
Februari 19, 2021 Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela alizungumza na Vyombo vya Habari na katika maelezo yake
alizishutumu mamlaka zinazosimamia mpira wa miguu kuwa haziitendei
haki klabu hiyo.
Baada ya kupitia shutuma hizo, Kamati imeona kuna haja ya mtoa shutuma kupewa haki ya msingi ya kusikilizwa na kuthibitisha madai yake mbele ya kamati husika.
Kutokana na hilo, Kamati inaliwasilisha suala
hilo TFF kwa ajili ya kupelekwa kwenye kamati yenye mamlaka ya
kusikiliza shauri hilo.
Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Februari 25, 2021