Connect with us

Makala

Kaze Afukuzisha Wawili

Timu ya Mwadui FC imeachana na kocha wake Khalidi Adam kutokana na mwenendo mbaya wa timu yao kwenye ligi kuu Tanzania bara hasa baada ya kufungwa mfululizo.

Uongozi wa Mwadui FC umefikia maamuzi hayo baada ya Jumamosi kufungwa 5-0 na Yanga SC ukiwa mwendelezo wa vichapo vya goli nyingi katika ligi kwa msimu huu wa 2020-21.

Mwadui ilifungwa 6-1 na JKT pia Simba SC waliwachakaza 5-0 uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na katika mchezo wa juzi Yanga nao waliwafunga mabao 5-0 ukiwa na ushindi wa kwanza mnono kwao.

Tangu atue nchini Cedric Kaze kocha mkuu wa Yanga SC amesababisha vibarua vya makocha wawili kuota nyasi huku akiweza kuiongoza vyema Yanga SC kuwachapa Azam FC 1-0 . Baada ya kipigo hicho Uongozi wa Azam ulivunja mkataba na kocha wake Cioaba kutoka nchini Romania.

Ushindi wa 5-0 ugenini dhidi ya Mwadui FC umepelekea klabu hiyo kumtimua kocha wake Khalid Adamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala