Connect with us

Makala

Shikhalo Kumpisha Ndalla Yanga sc

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa klabu hiyo ipo kwenye mpango wa kuachana na kipa wao raia wa Kenya, Faroukh Shikalo ili kupisha nafasi ya kusajili mchezaji mwingine wa Kimataifa.

Shikalo ameonekana kushindwa kumpa changamoto ya namba, Metacha Mnata ambapo Mkenya huyo mpaka sasa amesimama langoni kwenye mchezo mmoja pekee wa ligi msimu huu dhidi ya Tanzania Prisons ulioisha kwa sare ya bao1-1 mwanzoni mwa ligi.

Shikalo anatajwa kumpisha kiungo wa Plateau United ya Nigeria, Isah Ndala ambapo Yanga tayari wameambiwa dau la kiungo huyo ni Milioni 250 licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala