Connect with us

Soka

Yanga sc Kupaa Alhamis Kuifuata Mwadui

Klabu ya Yanga sc siku ya alhamis inatarajiwa kupanda ndege kuelekea mkoani Shinyanga kupitia Mwanza kwenda kuivaa timu ya Mwadui Fc mchezo wa ligi kuu utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Msafara huo wa klabu hiyo untarajiwa kuwa na watu 34 huku wachezaji wakiwa 24 viongozi 8 na waandishi wa habari 2 ambapo msafara utapitia mkoani Mwanza ambapo watatumia basi kufika Shinyanga.

Yanga sc inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujihakikishia mbio za ubingwa baada ya kuwa kileleni mwa msimamo na alama 34 katika michezo 14.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka