Connect with us

Makala

Azam Yapania Ubingwa Ligi Kuu Bara

Azam Fc iliyo chini ya kocha mkuu,Aristica Ciaoba imepania kuupata ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu wa 2020/2021 baada ya kujua mapungufu yao yapo wapi na kuyafanyia marekebisho.

Klabu hiyo iliyo na makazi yake chamazi inaongoza kwa sasa katika msimamo wa ligi kuu bara baada ya kucheza mechi nne huku ikishinda michezo yote na kujikusanyia pointi 12.

Azam imewaacha nyuma wapinzani wao Simba Sc na Yanga Sc kwa pointi mbili ambapo kwa sasa wameamua pia kuwaundia mikakati mizito timu hizo ili iendelee kushika usukani wa ligi na kuhakikisha wananyakuwa pointi tatu katika kila mechi.

Octoba 4,Jumapili Azam itakabiliana na Kagera Sugar katika raundi ya tano ya ligi kuu bara majira ya saa1:00 kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala