Connect with us

Makala

Tetesi Za Soka Ulaya

Taarifa zinaeleza kuwa Aston Villa ina mpango wa kumsajili beki wa kati wa Sampdoria,Omar Colley ambaye ni rafiki wa nahodha wa timu ya Taifa la Tanzani( taifa stars),Mbwana Samatta.

Colley ambaye alikuwa pamoja na Samatta katika klabu KRC Genk mwaka juzi anatazamwa kama mwarobaini wa kutibu safu ya ulinzi ya Aston Villa kutokana na uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

Sampdoria iliyochini ya kocha mkuu,Claudi Ranieri imeeleza kuwa inaweza kumuachia nyota huyo kwa kitita cha pauni milioni 18 ikiwa ni kama biashara itakayowaingizia faida kwani walimtoa Genk kwa pauni milioni 7.2

Kocha mkuu wa Aston Villa,Dean Smith anaonekana kuwa tayari kutoa dau hilo mezani kwani amekaririwa akisema kuwa, katika kipindi hiki cha usajili barani ulaya anahitaji kufanya uchaguzi sahihi wa wachezaji ambao anaamini watakuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi chao msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala