Connect with us

Makala

Sheria Yawakatili City Kumnyakua Messi Barca

Lionel Messi ametangaza kubakia Barcelona msimu wa 2020/2021 kutokana na ugumu wa masuala ya kisheria yaliyomo kwenye mkataba wake yanayomzuia kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Manchester City itakosa huduma ya nyota huyo waliokuwa wanaisubiria kwa hamu kubwa kwa msimu huu hivyo labda wasubiri tena msimu ujao ambapo ataweza kutoka barca akiwa mchezaji huru.

Messi Hajafurahishwa na kitendo cha kubaki Barcelona ila hofu kubwa aliyokuwa nayo hakutaka kuipeleka mahakamani timu iliyomlea kwenye soka hadi alipofikia sasa.

Mbali ya kuhofia suala la kufikishana mahakamani Messi anamlaumu sana rais wa klabu hiyo,Josep Maria Bartomeu kwani ameenda tofauti na makubaliano waliyopanga wakati anasaini Barca.

“Nilifikiria na niliamini kuwa nipo huru kuondoka kwani mara nyingi rais alikuwa akisema mwishoni mwa msimu naweza kuamua kubaki au kuondoka ,lakini wamenibadilikia baada ya kusema sikusema kabla ya June 10″alisema Messi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala