Connect with us

Makala

Serikali Waishauri Yanga Kuachana Na Morrison

Rais wa awamu ya nne wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Yanga kuachana na mvutano wa suala la mchezaji, Bernard Morrison kwani suala la kuibiana wachezaji kwa Simba Sc na Yanga Sc halikuanza hivi karibuni bali ni kawaida yao.

Kikwete ameyasema hayo jana kwenye kilele cha wiki ya mwananchi ampabo alialikwa kama mgeni rasmi kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa Mkapa.

“Kwa kuwa ninyi mmeibiwa Morrison najua nanyi mtajipanga wakati mwingine tena mtaiba mchezaji wao mzuri ni kawaida,Kinachotakiwa ni kuibua vipaji wenyewe ndani ili iwe rahisi kuwapata nyota ndani ya nchi ila masuala ya kupelekana FIFA ni kupoteza tu”alisema

Benard Morrison alitambulishwa kuwa mchezaji wa Simba kwenye kilele cha Simba day Agosti 22 Uwanja wa Mkapa huku Agosti 30 kwenye kilele cha wiki ya mwanachi alitambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga kwa kuwa shauri lake limepelekwa Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo,(Cas).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala