Connect with us

Makala

Simba Wabeba Taji Ngao Ya Jamii

Simba Sc imefanikiwa kutwaa taji la ngao ya jamii leo kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Wanamsimbazi hao wametwaa taji hilo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo Fc ambapo bao la kwanza lilipachikwa na John Bocco kwa mkwaju wa penalti dakika ya 7 baada ya Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18.

Bao la pili lilifungwa na Benard Morrison katika kipindi cha pili cha mchezo dakika ya 59 ambapo ushindi huo ulidumu dakika 90 za mchezo na kuifanya Simba kutwaa taji la ngao ya jamii mbele ya Namungo Fc inayonolewa na Hitimana Thiery.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala