Connect with us

Makala

Senzo Aanza Kazi Rasmi Yanga

Aliyekuwa mtendaji mkuu wa Simba Sc, Senzo Mbata leo Agosti 22 ameibuka ndani ya uwanja wa chuo cha Sheria kuwaona wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya wiki ya Wananchi pamoja na ligi kuu bara.

Yanga ilianza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2020/21 Agosti 10 na mchezo wake wa kwanza kwenye ligi unatarajiwa kuwa Septemba 6 dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Mkapa.

Senzo baada ya kuwasili mazoezini leo kwa mara ya kwanza alikutana na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Yanga Sc msimu huu kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko na wengine wengi.

Yanga Sc inatarajia kuwatangaza nyota wake wapya Agosti 30 kwenye kilele cha siku ya Wananchi ambapo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambapo timu ya Rayorn Sports inatajwa kutua kucheza na Yanga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala