Connect with us

Makala

Mo Dewji Ashindwa Kujizuia Kuhusu Wawa

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba Sc,Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ameamua kuziweka hisia zake wazi kuhusu beki mkongwe wa klabu hiyo Pascal Wawa kutokana na ubora wa kiwango chake ndani ya kikosi.

Wawa ambaye ni beki wa kati ameichezea Simba misimu miwili ambayo  imetwaa ubingwa mfululizo akiwa kwenye kiwango kizuri ingawa anaonekana kuwa mchezaji mkongwe wa soka.

Mo Dewji amemwaga sifa nyingi kuhusu beki huyo katika ukurasa wake wa Instagram akisema “Pascal Wawa juhudi na nidhamu vimeendelea kukufanya kuwa bora kadri muda unavyoenda, nafasi ya beki huambatana na lawama nyingi kuliko pongezi lakini haijawahi kukusumbua wala kukupotezea umakini uwanjani.

“Nathamini mchango wako na nina imani utaendelea kuwa sehemu muhimu ya Simba kuweza kufikia malengo yetu msimu ujao! Good interview Pascal”aliongeza Mwekezaji huyo wa Simba Sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala