Connect with us

Makala

Kissu Amwaga Wino Azam Fc

David Mapigano Kissu ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Azam Fc baada ya kusaini kandarasi  ya miaka miwili akitokea klabu ya  Gor Mahia ya Kenya.

Kissu alichezea timu za Njombe Mji na Singida United kabla ya kutimkia nchini Kenya pia alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kabla ya janga la virusi vya Corona halijasimamisha masuala ya michezo.

Akiwa na Gor Mahia amecheza jumla ya mechi 15 huku akiwa hajaruhusu nyavu zake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo na timu yake ilitangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Kenya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala