Connect with us

Soka

Tp Mazembe Kuwatoa Ambokile,Singano

Taarifa kutoka DR Congo zinasema kuwa klabu ya TP Mazembe inampango wa kuwatoa kwa Mkopo wachezaji wao Raia Tanzania Mshambuliaji Hatari Eliud Ambokile Pamoja na Kiungo Hatari Ramadhani Singano Katika Dirisha lijalo la usajili.

Ambokile alijiunga na klabu ya TP Mazembe akitokea katika klabu ya Mbeya City Huku mwezake Ramadhani Singano alijiunga na wababe hao akitokea katika klabu ya Azam FC.

Mpaka sasa nyota hao wamekosa nafasi ya Kucheza katika kikosi cha Kwanza cha wababe hao wa DR Congo na haijafahamika kama timu za hapa nchini zimeonyesha nia ya kuwasajili mastaa hao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka