Connect with us

Soka

Simba sc,Yanga sc Zamlilia Mkapa

Klabu kongwe za soka nchini Tanzania Simba sc na Yanga SC zimeomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kwa masikitiko makubwa kufuatia mchango wa Rais huyo katika michezo nchini.

Klabu hizo kupitia mitandao yao ya kijamii zimechapisha picha na maneno yanayoonyesha masikitiko kufuatia kifo cha mstaafu huyo aliyekua Rais wa tatu wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania huku pia akiwa na Rais mwanzilishi wa mfumo wa Vyama vyingi nchini.

“Young Africans Sports Club tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha rais wa awamu ya tatu ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania” ilisomeka taarifa kutoka mtandao wa instagram wa klabu ya Yanga.

Pia kwa upande wao mabingwa mara tau mfululizo klabu ya Simba sc ilisomeka hivi “Simba sc tunatoa pole kwa familia,ndugu,marafiki na watanzania kufuatia msiba huu mkubwa kwa watanzania.Tunaiombea roho ya marehemu ailaze mahala pema peponi amina.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka