Connect with us

Soka

Yanga Mtelezo Kimataifa

Upo uwezekano mkubwa kwa Tanzania kupata nafasi nne za uwakilishi kwenye michuano ya vilabu barani Afrika (CAF CL na CC) kutokana na uwezekano wa Libya kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kukosa sifa kwa kuwa hawakuendesha ligi yao kutokana na changamoto za kiusalama.

Kupitia michuano inayoendelea msimu huu, Libya iliweza kuipiku Tanzania miongoni mwa nchi zenye sifa ya kutoa timu nne kwenye michuano hiyo baada ya kufikisha alama 16.5 wakati Tanzania ikishuka nafasi ya 13 ikiwa na alama 14.

Hata hivyo kulingana na kanuni za CAF nchi ambayo haitaendesha ligi yake kwa angalau msimu mmoja inapoteza nafasi zake.

Aidha nchi za Ethiopia, Sudan Kusini na Jamhuri za Afrika ya Kati nazo zimetangaza kujiondoa kushirikia michuano hiyo msimu ujao na hivyo kuongeza matumaini ya Tanzania kurudishiwa nafasi zake nne.

Kama hili litatokea, klabu za Yanga na Azam Fc zitaungana na Simba na Namungo Fc ambazo tayari zimekata tiketi. Timu itakayomaliza nafasi ya pili itacheza ligi ya mabingwa wakati ile itakayomaliza nafasi ya tatu itacheza kombe la Shirikisho.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka CAF ingawa amekiri kuwa taarifa ya Libya kuondolewa kwenye michuano hiyo wameiona mtandaoni.

Katika orodha ya nchi iliyotolewa na CAF zenye sifa ya kutoa timu nne, Libya haimo licha ya kushika nafasi ya 12 juu ya Tanzania inayoshika nafasi ya 13.

Cc:Mitandao

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka