Connect with us

Soka

Mwakyembe Apigwa Chini

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr. Harison George Mwakyembe ameshindwa kwenye kura za maoni kuteuliwa kugombea Jimbo la Kyela Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwakyembe amekuwa Mshindi wa Tatu Baada ya kupata kura 252 huku Mshindi wa Pili Hanta Albert Mwakifuna akipata kura 288 na kwanza ni Ally Mlagila Jumbe (Kinanasi) (Mwenye suti nyeusi katikati) akipata kura 502.

Hata nafuu aliyonayo Waziri huyo wa michezo ni kusubiri Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambayo itakaa na kupitia majina ya washindi hao ili kuyapitisha ambapo pia mgombea aliyeshinda kura za maoni anaweza asipitishwe kusimamishwa kama mgombea wa chama.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka