Connect with us

Soka

Mbeligiji Amkataa Gadiel Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema tetesi za kuwa wako mbioni kumsaji beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michael hazina ukweli wowote huku akisema tayari nafasi hiyo ishajazwa na staa wa kigeni.

Eymael amesema sio Gadiel tu, bali hawana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote kutoka klabu ya Simba

“Hapana ,tulishasajili mlinzi wa kushoto ambaye anatoka nje nchi pia hatujawahi kumtaka mchezaji yoyote kutoka ndani ya kikosi cha Simba,” amesema Eymael

Tangu jana tetesi zinazomuhusisha Gadiel kutaka kurejea Yanga zimeripotiwa sana kwenye mitandao ya kijamii

Gadiel aliondoka Yanga katika mazingira ambayo hayakuwafurahisha mabosi wa timu hiyo akienda kujiunga na Simba

Alipewa mkataba kabla ya kwenda kushiriki michuano ya Afcon na kikosi cha Stars nchini Misri hata hivyo hakuusaini mkataba huo na akasubiri siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa akatangaza kujiunga na Simba

Mashabiki wa Yanga wameonekana kuchukizwa na tetesi za mchezaji huyo kuhusishwa na mabingwa hao wa kihistoria kutokana na matukio aliyofanya msimu uliopita.

Cc:Sokaonline

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka