Connect with us

Soka

Azam Yasimamishwa Samora

Harakati za klabu ya Azam fc kumaliza nafasi ya pili ligi kuu Tanzania bara zimesimamishwa na klabu ya Lipuli Fc baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 uwanja wa Samora Mkoani Iringa.

Azam Fc walikua wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdalah Kheri dakika ya 44 lakini walishindwa kulilinda bao hilo na kusawazishwa na Paulo Materazi dakika ya 80 na mchezo kumalizika kwa timu hizo kugawana pointi.

Azam fc imesalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili juu ya Azam fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka