Connect with us

Makala

Nani Mbabe Wao?

Kesho katika viwanja saba tofauti ligi kuu bara itaendelea huku yanga ikiwa mbioni kuzisaka pointi tatu mbele ya Mwadui Fc Uwanja wa Taifa Jijini Dar-es-salaam.

Yanga Sc wanashika nafasi ya pili kwa sasa wakiwa wana pointi 67 ambazo walizipata Jumatano dhidi ya Singida United huku wapinzani wao Azam Fc wakiwa nafasi ya 3 na pointi 65.

Azam ambayo inatarajia kuingia uwanjani Jumapili dhidi ya Lipuli Fc itatamani Yanga wapoteze mchezo wa kesho na wao washinde ili waweze kuwa na pointi 68 na warudishe nafasi yao ya pili lakini kama wote watafanikiwa kushinda michezo hiyo watabaki kwenye nafasi zao,Yanga ikiwa na pointi 70 huku Azam Fc pointi 68.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala