Connect with us

Makala

Mwenyekiti Simba Awania Ubunge Kinondoni

Aliyekuwa mwenyekiti ndani ya Simba Sc ,Swedi Mkwabi ametia nia katika uchukuaji wa fomu ya kuwania ubunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar-es-salaam ,siku ya leo katika ofisi za chama cha mapinduzi (CCM) zilizopo Mkwajuni.

Mkwabi alilazimika kuachia nafasi hiyo ya uwenyekiti Septemba mwaka jana baada ya kuwa na mambo mengi yaliyomfanya kuwa bize zaidi ya kuitumikia klabu hiyo.

“Nimechukua uamuzi huu kwa sababu ni haki yangu ya kikatiba kama mwananchi na mwanachama wa chama cha mapinduzi ,nimejipima na kuona natosha katika nafasi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa Kinondoni”alisema Mkwabi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala