Connect with us

Soka

Nemanja Matic Mpaka 2023

Kiungo mkongwe wa klabu ya Manchester United Nemanja Matic amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2023.

Staa huyo alijiunga na Man united mwaka 2017 akitokea Chelsea na kufanikiwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha mashetani wekundu kilichokua kikiongozwa na Jose Mourinho ambapo hata Ujio wa mkufunzi Ole Gunnar Solskajaer ameendelea kumtumia.

“Nina furaha kuendelea kuwa sehemu ya klabu hii kubwa,kama mchezaji nina mengi ya kutoa na kushinda katika soka langu na ni heshima kubwa kufanya hivyo na Manchster United” Alisema Nemanja Matic.

“Nina furaha kwamba Nemanja amesaini mkataba mpya,Nafahamu uzoefu wake,Taaluma yake na uongozi vitakua na thamani sana kwa vijana haya wadogo wenye vipaji” Olle Gunnar Solskjaer.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka