Connect with us

Soka

Sancho Akubali Kutua Man United

Taarifa kutoka nchini Ujerumani zinaripotiwa kuwa Jodan Sancho amekubali kujiungua na Manchester United na atasaini mkataba wa miaka 5 kwenye dirisha la usajili la majira ya joto yaliyoanza hivi sasa.

Lakini, kitu kinachokwamisha deal hilo mpaka sasa ni kiasi ambacho Dortmund wanakitaka £100million. Huku inaelezwa kuwa United hawako tayari kutoa zaidi ya £50

Inaaminika kuwa Sancho ndio mchezaji ambaye United wanamuhitaji zaidi kwenye dirisha la majira ya joto, huku Ole Gunnar Solskjaer anataka kuongeza ubunifu ndani ya kikosi chake na anaamini kuwa Sancho ni suluhisho.

Muingereza huyo pia anawindwa na Chelsea , huku kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema anampango wa kumsajili Sancho ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo japo  United ndio wanapewa nafasi kumbwa ya kumpata Jodan ambaye amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake.

Sancho msimu huu kwenye Bundesliga amehusika katika mabao 34 ambapo ametoa assist 17 na kufunga mabao 17 katika michezo 32.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka