Connect with us

Soka

Rasmi Simba vs Yanga

Klabu ya Simba sc itakutana na Yanga sc katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho baada ya kufanikiwa kuifunga Azam fc mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Simba sc walitawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Nahodha John Boko dakika ya 40 akifunga kwa kichwa kupitia pasi ya juu ya Francis Kahata Nyambura bao lililodumu hadi mapumziko.

Iliwachukua Simba sc dakika 10 za kipimdi cha pili kuandika bao la pili kupitia kwa Mwamba wa Lusaka Cletous Chama aliyefunga bao zuri kupitia pasi ya Shomari Kapombe.

Matokea hayo yanamaanisha kuwa Simba sc itakutana na Yanga sc ambayo ilimfunga Kagera Sugar kwa mabao 2-1 huku nusu fainali nyingine ni Namungo Fc dhidi ya Sahare All Stars.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka