Connect with us

Soka

Yanga,Azam Hakuna Mbabe

Hakuna mbabe ndilo neno rahisi unaloweza kulitumia baada ya mechi baina ya Yanga sc dhidi ya Azam fc kumalizika kwa suluhu licha ya mashambulizi makali kutoka pande zote.

Azam fc walikaribia kupachika mabao mawili kipindi cha kwanza lakini juhudi za kipa Metacha Mnata ziliwanyima mabao huku pia Sibomana na Molinga nao walikosa nafasi kadhaa za wazi.

Licha ya Benard Morrison kuleta kashikashi dakika za mwanzo kipindi cha pili Azam fc walifanikiwa kumdhibiti baada ya kumuingiza Bruce Kwangwa.

Azam fc watasilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 huku Yanga wakiwa na pointi 55 katika nafasi ya tatu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka