Connect with us

Soka

Molinga,Yikpe Matatani

Mastaa wa klabu ya Yanga David Molinga na Yikpe Gnamien wameingia matatizoni baada ya kukutwa na uzito uliopitiliza baada ya kurejea mazoezini na timu wiki hii.

Mastaa wote wa klabu hiyo walifanyiwa vipimo vya afya wakati wanarejea mazoezini chini ya Madaktari ili kujua utimamu wa miili yao baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia kusambaa kwa virusi vya Corona nchini hivyo kuilazimu serikali kusimamisha shughuli za michezo nchini.

Ripoti hiyo inaonyesha Molinga ameongezeka kilo kumi na mbilikutoka zile za awali huku Yikpe akiongezeka kilo kumi na Patrick Sibomana amekutwa na uzito uliongezeka kilo saba.

Mastaa hao watakutana na kibano kutoka kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Luc Eymael ambae aliacha programu maalumu ya mazoezi ambayo mastaa hao walitakiwa waifuate hivyo kuongezeka uzito kunamaanisha kuwa hawakufuata maelekezo ya mwalimu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka