Connect with us

Makala

Kisa Madoli,Fc Soul Yaomba Radhi

Klabu ya FC Seoul nchini Korea Kusini imeomba msamaha kwa kutumia madoli na kuyafanya mashabaki ili kujaza viti ambavyo kwa kawaida hukaliwa na mashabiki wanaofika uwanjani kuhudhuria mechi .

Shughuli za soka zimeanza kurejelewa katika baadhi ya mataifa kama vile Ujerumani, Korea Kusini na Belarus licha ya janga la corona kutodhibitiwa vilivyo duniani, japo mchezo huo wa mpira wa mguu unaopendwa sana utakuwa ukipigwa ndani ya viwanja vitupu bila mashabiki .

FC Seoul ilijaza madoli kwenye viti vya uwanja wao wa nyumbani mnamo Mei 17, 2020, kabla ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Gwangju FC ila  ilihitaji macho makali ya mashabiki kutambua kwamba madoli hayo yalikuwa ya mapenzi.

Ingawa cha kushangaza ni jinsi mashabiki walivyoweza kubaini kwamba madoli hayo hutumiwa katika masuala ya ngono, na viongozi wa FC Seoul wamekiri makosa na kutumia mtandao wa Instagram kuomba radhi huku wakishikilia kwamba mkandarasi aliyetakiwa kuupamba uwanja wao kwa madoli ya kawaida, alichanganyikiwa.

Lengo la klabu hiyo ya Fc Soul ya kutumia madoli ni kutangaza jezi ambayo madoli hayo yalikuwa yamevaa ingawa imeleta tafsiri mbadala kwa mashabiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala