Connect with us

Makala

David Silva Apiga Hesabu Kurejea Valencia

Nyota wa kikosi cha Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu England,David Silva amesema kuwa hatakuepo ndani ya timu hiyo msimu ujao wa 2020/21 kwani anaweza kurejea ndani ya timu yake ya zamani ya Valencia huko Hispania.

Kiungo huyo mwenye miaka 34 amesema kuwa hana mpango wa kuendelea kubaki ndani ya kikosi hicho cha Man City msimu ujao pale mkataba wake utamalizika ingawa inaelezwa kuwa City ilitumia nguvu kubwa kumbebeleza nyota huyo abaki ndani ya klabu hiyo ila aligoma kufanya hivyo kwa kuamini kuwa muda wake wa kufanya hivyo umefika.

Manchester City ipo nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu England ikiwa na pointi 57 huku Liverpool ikishika nafasi ya kwanza na pointi 82 kibindoni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala