Connect with us

Makala

Corona Yamkosesha Amani Manara.

Afisa  habari wa klabu ya Simba Sc, Haji Manara amefunguka kuwa anakosa amani kwani kila anapowaza janga la virusi vya Corona hajui litakwisha lini pia anafikiria kama itawezekana tena dunia kurudi katika hali yake ya kawaida na watu kuendelea na shughuli zao kama ilivyokuwa awali bila kuwa na hofu zaidi.

Manara aliweka sauti kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa, “hivi tutarudi na watu tukaaminiana bila ya kukwepana, watu wataingia misikitini, makanisani kufanya ibada bila hofu?”

“Walimwengu mimi nina hofu sana, siku ya tatu hii najiuliza hili swali, hamuoni kama kuna jambo Mwenyezi Mungu anataka kutufundisha kitu kupita kwa haya maradhi aliyotuletea?sayansi itakataa ila mimi naamini ipo sababu ya Mungu katika jambo hili” alisema Manara.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala