Connect with us

Makala

Shonga Kushushwa Yanga,Morrison

Nyota Mghana wa klabu ya Yanga Sc, Benard Morrison amebainisha kuwa na uwezo wa kumshawishi Justine Shonga wa Orlando Pirates kuungana na kikosi cha Yanga endapo viongozi watakuwa tayari kumpatia mchezaji huyo kiasi cha fedha anachokihitaji.

Morrison ni mchezaji aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili katika timu ya Yanga pia amekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya timu hiyo hasa baada ya kuisaidia kushinda dhidi ya Simba .

Kiungo huyo amesema kuwa yupo tayari kuisadia Yanga kwenye maongezi yao na Shonga kwani ni mchezaji ambaye wanafahamiana na walishawahi kuwa pamoja Orlando Pirates kabla ya kujiunga na Yanga.

“Nipo tayari kuzungumza na Shonga kwani ni mda mrefu sasa naona kama hana nafasi sana kwenye kikosi cha kwanza japo uwezo wake ni wa hali ya juu”alisema Morrison

Aliongeza kuwa endapo yanga wakimuhitaji na kumpatia dau analotaka mimi hatakuwa na kipingamizi cha kuwasaidia kwani akija atakuwa msaada mkubwa kwake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala