Connect with us

Makala

Mmiliki Wa Ihefa Fc Afariki

Ihefa fc Imepata pigo kubwa baada ya kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa mmoja wa wamiliki wa timu hiyo,Abdulhaq Pirmohamed.

Mmiliki huyo alianza kuugua siku kadhaa kabla ya umauti kumkuta siku ya jana Alhamisi,wakati alipofanyiwa upasuaji aligundulika kuwa na mawe kwenye figo.

Wakati wakimfanyia upasuaji mgonjwa alipata mshtuko wa moyo ambapo ilibidi madaktari kutumia njia mbadala kumsaidia kupumua,lakini licha ya juhudi zote kufanyika hali ilibadilika jana ghafla na akaaga dunia alfajili ya jana na kuzikwa siku hiyohiyo kwenye makaburi ya kisutu,Dar-es-Saalam.

Ihefa Fc ligi daraja la kwanza (FDL) inashika nafasi ya pili kundi A kwa pointi 39 sawa na Dodoma inayoongoza msimamo kwa uwiano mzuri wa mabao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala