Staa wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes amekubali uwezo wa staa wa klabu hiyo Paul Pogba ambaye alikua nje ya uwanja kutokana na majeraha ya mguu.
Bruno ambaye toka amesajiliwa united hajapata nafasi ya kucheza pamoja na staa huyo wa zamani wa Juventus amesema anangojea kwa hamu muunganiko wao ili waisaidie timu hiyo kwa maana kila mmoja ana aina yake ya uchezaji.
“Mimi ni mchezaji ambaye hupenda kujitolea zaidi, pia napenda kutoa pasi za mwisho na jaribu kutoa msaada zaidi kwa wachezaji wenzangu kwa hivyo ninahitaji kujitolea zaidi.
“Tunaweza kuzungumza juu ya kuleta wachezaji wapya lakini hatujaona kabisa Pogba akicheza kwa kufurahia labda kwa sababu moja au nyingine labda akirejea itaonekana nafasi ya kuletwa mchezaji mwingine.
“Alikuwa na majeraha, lakini wakati huo huo mimi namtarajia kumuona akirudi tupeane changamoto mpya tunatazamia kuona ushirika mzuri lakini pia huo ushirikiano unaileta nini klabu kwa sababu Paul anataka kucheza bora zaidi na kuonyesha matunda yake baada ya kuwa nje Kwa kweli ni kitu cha kutarajia. ” “Namjua Pogba tangu yuko Juve kwa sababu nilicheza naye huko, Ni ngumu kupata mchezaji kama yeye ni hodari uwanjani kiufundi. Niamini, ni ngumu sana kumkaba Paul”Alimalizia kiungo huyo ambaye usajili wake umekua na mafanikio Old Traffod.