Connect with us

Soka

“Tukipata Wanne Fresh”-Scholes

Kiungo wa zamani wa Man Utd Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United bado inahitaji wachezaji wengine wasiopungua wanne ili kuwa kwenye viwango vya kuchuana Liverpool kwenye Ligi Kuu England, licha ya staa wao mpya, Bruno Fernandes kufanya maajabu tangu alipotua Old Trafford Januari.

“Bado nadhani kuna wachezaji wanahitaji. Wameonekana wazuri kwa siku za karibuni tangu alipokuja Fernandes, lakini Liverpool na Man City wapo mbali sana,” Alisema kiungo huyo ambae wakati anacheza hakua na wakala wa kumsimamia.

Mastaa kibao wamehusishwa kuhitajika Old Traffod kwenda kujenga kikosi cha kurudisha zama za ushindi klabuni hapo kama Jadon Sancho,Thomas Weimer,Harry Kane na wengineo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka