Connect with us

Soka

Njombe Mji Ipo Sokoni

Wiki moja iliyopita uongozi wa klabu ya Njombe Mji ulitangaza mpango wa kuipiga bei klabu hiyo, mchakato huo bado unaendelea lakini hadi sasa bado hajapatikana mteja ambaye yuko tayari kutaka kuinunua.

Kwa mujibu wa Kaini Nyigu, afisa habari Njombe Mji FC mpaka sasa hakuna mnunuzi aliyejitokeza kununua klabu hiyo.

“Mpaka hivi sasa siku 7 zimepita ambazo zilikoma tangu Machi 30 tangu tulipotangaza kuiuza klabu ya Njombe Mji FC (Machi 22, 2020) lakini hakuna mteja aliyejitokeza. Kamati ya utendaji bado wanawaomba watu kadhaa ili waweze kuinunua”.

“Tutatangaza kama mtu amejitokeza kutaka kuinunua lakini timu bado ipo sokoni inaendelea kuuzwa kwa maazimio ya wanachama.”

Timu hiyo ipo sokoni ambapo mnunuzi lazima akubali kufuata masharti yakiwemo kutobadilisha jina la kwanza la klabu  ambalo ni Njombe huku pia Hatakiwi kuitoa timu nje ya mkoa wa Njombe (unaweza kuitoa wilaya moja kwenda nyingine ndani ya mkoa wa Njombe) na sharti la mwisho ni  Wanachama lazima waendelee kuwa na hisa ndani ya klabu.

Credit:shaffihdauda

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka