Connect with us

Soka

Manula Ampa Tano Morrison

Kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Simba Aishi Manula amempongeza staa wa klabu ya Yanga Benard Morrison baada ya kumfunga bao katika mechi baina ya watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba.

Katika mchezo huo dakika ya 44 Morrison alipiga faulo iliyoenda moja kwa moja langoni na kumuacha kipa huyo akiwa anashangaa kutokana na kasi na ufundi uliotumika kupiga mpira huo.

Akihojiwa na kituo kimoja cha radio nchini Kipa huyo alimpongeza mpigaji baada ya kutumia akili kupiga mpira huo uliokua na kasi huku ukifanikiwa kuwapita mabeki wa klabu hiyo.

Bao hilo liliwafanya Yanga kupata ushindi wa kwanza baada ya miaka minne katika pambano la watani wa jadi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka